Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake anaponza nan a wema wake alionao kama lilivyokuwa jina lake.

Hayo yamekuja hivi karibuni baada ya msanii na prodyuza wa Bongo Fleva, Bob Junior kudai kuwa yupo kwenye uchumba na Wema akijipanga kwenda kumtolea posa, jambo ambalo limemboa mno mrembo huyo.

Wema amekuwa akilalamika kutumiwa kama daraja la kuwapa watu ustaa, lakini yote ni kutokana na wema na upendo wake kwani kila anapokutana na mtu huwa anamuonesha upendo ambao wengine huutumia vibaya kwa kudai kuwa wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi.

“Kile kitendo chake cha kumuona mtu ambaye labda hajamuona kwa muda mrefu na kumkarimu kwa kumkumbatia na kumbusu, lakini wengine wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kwa manufaa yao binafsi kama alivyofanya Bob Junior.

“Ifike kipindi watu wamuheshimu Wema, kama mtu anahitaji kiki, basi Wema ni mtu wa watu, hawezi hata kutoza pesa kwa ajili ya kiki, ishu ni kwenda na kumuambia nina projekti yangu, naomba unibusti kuliko kuibua mambo mengine kama hayo ya kwenda kumtolea posa, wakati Wema ana mtu wake.

“Naomba watu wamuheshimu Wema hata kidogo, anavyowakarimu na kuwakumbatia, basi na ninyi muoneshe heshima kwake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *