Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amedai kuwa dawa ambazo anatumia ndiyo zinamponza kuwa na mwili mkubwa ambao yeye mwenyewe haupendi na kusema kuwa kwa sasa anatamani kuziacha ili aweze kupungua mwili wake.
Wema Sepetu ameweka wazi hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Instgram wakati akimjibu msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Ray C ambaye ameweza kufanikiwa kupunguza mwili wake na kilo na kurudi kwenye ubora wake kama zamani.
Ray C alikuwa akiwakumbusha Shilole pamoja na Wema Sepetu kuwa wanaweza kupunguza miili yao na kilo na kuwa kama zamani kwa kujitolea mfano yeye.
Kufuatia kauli hiyo ya Ray C ndipo mwanadada Wema Sepetu alipoamua kuweka wazi kuwa si mapenzi yake yeye kuwa na mwili huo alionao sasa bali ni kutokana na matumizi ya dawa, ambazo hakuweka wazi ni dawa zipi, ingawa baadhi ya mashabiki wameunganisha na kudai kuwa huenda msanii huyo anatumia dawa zitakazomsaidia ili aweze kuja kushika ujauzito, huku wengine wakisema ni matumizi ya dawa za kupunguza mwili.
Baada ya jibu hilo Ray C alirudi tena na kumpa pole Wema Sepetu na kumweleza kuwa hakuna namna tena inabidi azikate ili aweze kupungua na kudai kuwa inawezekana kabisaa Wema Sepetu akarudi kama zamani endapo atazingatia mafunzo, mpangilio mzuri wa chakula na kusema kabla ya mwaka atampa matokeo ya hilo.