Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amefanya ziara nchini Marekani na kupokelwa na mwenyeji wake Donald Trump ambapo watasafiri kwenda Florida wakitumia ndege yake Air wikiendi hii.

Katika mazungumzo yao Trump amemhakikishia kiongozi huyo kuhusu kuendelea kusaidia kudumisha usalama wa Japan na kwamba uhusiano wao ni nguzo muhimu kwa amani na utulivu wa eneo la Asia Pacific.

Trump ametoa hakikisho kwamba majadiliano ya kibiashara baina ya Marekani na Japan yatakuwa ya uwiano mzuri wa kufaidi mataifa yote mawili.

Kwa upande wake waziri mkuu Abe amesema pia wamekubaliana kulipa kipau mbele swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia vinavyotolewa na Korea Kazkazini..

Pia amesema kuwa mazungumzo yao ya baadae leo yatalenga kuchambua zaidi mkataba wa kibiashara wa Trans-Pacific ambao Trump amekuwa akisema Marekani haina nia ya kuuendeleza .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *