Mattis yupo nchini Korea Kusini ambapo ameihakikisha Seoul Korea kwamba inaungwa mkono na Marekani.
Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini mbali na taarifa za uchokozi yanaendelea kutia wasiwasi mbali na kuyakasirisha mataifa ya eneo hilo.
Marekani ina wanajeshi wengi nchini Korea Kusini na Japan ikiwa ni mpango wa ulinzi wa baada ya vita.
Rais Donald Trump awali amenukuliwa akisema kuwa mataifa hayo mawili yanafaa kuilipa Marekani zaidi ili wanajeshi wake kusalia kukaa nchini humo.
Bw Mattis ametumia ziara yake nchini Korea Kusini kulihakikishia taifa hilo kwamba utawala wa bw Trump utaendelea kulinda eneo hilo.