Waziri wa haki nchini Gabon, Seraphim Moundounga amejizulu kulalamikia utata ambao umegubika matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo wiki moja iliyopita.

Waziri huyo amemuonya Rais Ali Bongo ambaye alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi kwamba angefuta matokeo ya uchaguzi huo iwapo hayatalingana na uhalisia.

Bw Mondunga ndiye afisa wa juu serikalini kujiuzulu kufuatia mzozo huo kuhusu matokeo ya uchaguzi.

Mamlaka za Gabon zimesema watu watatu wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye ghasia ambapo pia maelfu wamekamatwa.

Baadhi ya taarifa zinasema huenda idadi ya raia waliokufa ikawa juu kuliko inayosemwa sasa nchini humo.

Ufaransa imelalamikia hali inayoendelea nchini Gabon na kusema baadhi ya raia wake nchini humo hawajulikani waliko.

Ali Bongo alitangazwa mshindi wa uchaguzi lakini upinzani ukiongozwa na Jean Ping ulipinga matokeo.

Bw Bongo alipata 49.8% ya kura naye Bw Ping akiwa na 48.2%, tofauti kati yao ikiwa kura 5,594.

Bw Ping alishinda majimbo sita kati ya tisa na ameomba kurudiwa tena kwa shughuli ya hesabu ya kura.

Katika jimbo la Haut-Ogooue anamotoka Bw Bongo waliojitokeza kupiga kura walikuwa 99.93%  kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na 95% ya kura zilimpigiwa rais huyo.

Idadi ya wapiga kura waliojitokeza majimbo mengine ni 45% na 71%, kwa mujibu wa wizara ya masuala ya Gabon.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *