Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), kubaini baadhi ya walimu kuishi nchini bila vibali.
Katika ziara hiyo iliyofanyika leo Profesa Ndalichako ameambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala.
Wengine aliongozana nao ni mkuu wa Ithibati na Udhibiti Ubora wa Vyuo, Dk Valerian Damian na maofisa mbalimbali kutoka idara ya uhamiaji na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Profesa Ndalichako amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwamo walimu wa chuo hicho kuajiriwa sehemu zaidi ya moja na kuishi nchini bila vibali.