Waziri wa Afya Maendeleo yajamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekemea tabia ya wakuu wamikoa na wakuu wawilaya kuwaweka ndani  ama kutoa adhabu mbalimbali kwa madaktari wanaokiuka taratibu.

Waziri Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais kuhutubia kongamano la 49 la Chama Cha Madaktari nchini ambapo Ummy Mwalimu amesema endapo daktari akikosea nivyema akapelekwa kwenye baraza la madaktari kujadili ni adhabu gani anapaswa kupatiwa kulingana na kosa alilolifanya kudhibitika kitaaluma.

 Hata hivyo Waziri huyo ametolea mfano kama wagonjwa kulaumu, mama mjamzito kupoteza maisha kuwa ni muhimu taaluma ikachunguza kuliko kutoa adhabu kabla mabaraza ya udaktari.

 Hata hivyo Waziri Ummy ameongeza kuwa ni busara kufuata hatua za kiuwajibikaji na sio kujiamulia adhabu ya kuwapa madaktari bila kuthibitisha  makosa wanayowatuhumu nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *