Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu amewaonya Wakurugenzi wote wa Halmashauri watakaokaidi agizo la Serikali la kutenga asilimia 4 kwa ajili ya wanawake na vijana pamoja na asilimia 2 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Rukwa ambapo amepokea changamoto kutoka kwa wanawake wengi kuhusu utoaji mdogo wa mikopo na wengine kutopata kabisa mikopo kutoka Halmashauri zao.

Ummy amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kutenga asimilia 4 kwa ajili ya wanawake na kutoa mikopo yenye tija itaakayoweza kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na sio kurudi nyuma kiuchumi.

Aliongeza kuwa ili kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda basi Halmashauri hazina budi kujiwekea mikakati ya kutoa mikopo mikubwa itakayo wawezesha wanawake na wananchi kwa ujumla kufikia dhana hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula ameiomba Serikali kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwapa elimu ya jinsi ya kutumia fedha na kuendesha miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Khalfan Haule amesisitiza wadau kushirikiana na Serikali pale ambapo wanaweza kuwawezesha wanawake sehemu walipo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchangokatika kuchangia kujiletea maendeleo jumuishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *