Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amewapa somo wakurugenzi wapya walioteuliwa hivi karibu na kuapishwa jana mjini Dodoma.
Waziri huyo amewataka wakurugenzi hao kuacha kufanya na mitandao ya kijamii kwa kuwa imekuwa ikitoa taarifa ambazo siyo sahihi.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini humo alipokuwa akizungumza na wakurugenzi hao baada ya kuapishwa. Alisema:
Waziri huyo alitoa mfano wa taarifa iliyotolewa katika mitandao ya jamii hivi karibuni kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi imeanza kuwaruhusu waombaji wa ajira za ualimu kuanza kutumia mfumo wa maombi ya ajira za ualimu(On line Teachers Employment Application System-OTEAS) kuwa siyo za kweli.
Aliwataka wakurugenzi hao kutokaa ofisini na badala yake waende kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.
Wakurugenzi walioapishwa na Halmashauri zao katika mabano ni Mwantumu Dau (Bukoba), Frank Bahati (Ukerewe), Hudson Kamoga (Mbulu), Mwailwa Pangani (Nsimbo), Godfrey Sanga (Mkalama) na Yusuph Semuguruka(Ulanga).
Wengine ni Bakari Mohammed (Nachingwea), Juma Mnweke (Kibondo), Batamo Ndalahwa (Moshi), Waziri Mourice (Karatu), Fatma Latu (Bagamoyo), Godwin Kunambi (Manispaa Dodoma) na Elias Ntiruhungwa (Tarime Mjini).