Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza wakuu wote wa vyuo nchini kuwatambua wanafunzi wao wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni mjumbe wa Tume ya Kudhibiti Dawa ya kulevya kutokana na wadhifa wake ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao cha kazi cha wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDCs) .

Amesema agizo hilo amelitoa kwa wakuu wa vyuo vyote nchini kuona kuwa wanakuwa makini kuhakikisha kuwa vyuo vyao havigeuzwi kuwa vijiwe vya watu wanaotumia madawa ya kulevya.

Pia waziri huyo amesema kuwa vijana wengi walioko vyuo vikuu wameharibikiwa kutokana na madawa ya kulevya hivyo nguvu kubwa inahitajika katika mapambano hayo ili kulinusuru taifa.

Mwisho waziri huyo ameviagiza vyuo vya maendeleo ya Wananchi kuhakikisha kuwa vinajitangaza kwa jamii ili vionekane kuwa vipo kwa kuwa vyuo vingi havina wanafunzi wa kutosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *