Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi wizara yake pamoja na kamati ya ulinzi mkoa na wilaya zinaimarisha ulinzi katika maeneo yaliyokumbwa na janga hilo.
Ametoa kauli hiyo leo bungeni mjini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa kuhusu usalama wa wahanga hao.
Waziri huyo amesema “Kwakuwa watu ni wengi inatokea katika kutafuta namna ya kujiridhisha kujua yupi anaenda kwa kutoa huduma na nani anaenda kwaajili ya kukwapua ama kuchukua vile ambavyo vimezagaa zagaa, kwahiyo ndio maana utaona mwingiliano wa aina hiyo,”.
Pia ameongeza kwa kusema “Nia ya wizara pamoja na kamati za ulinzi na usalama za wilaya, ni kuhakikisha hao waliopata matatizo wao pamoja na mali zao wanakuwa katika hali ya usalama,.
Jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliendesha harambee ya kuwachangia wahanga wa tetemeko hilo.
Takriban shilingi bilioni 1.4 zilichangwa kutokana na harembee hiyo iliyoendeshwa na Waziri mkuu hapo jana.