Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa wizara yake inafuatilia tukio la kutekwa kwa mwanamuziki Roma.
Kauli hiyo aliitoa mjini Dodoma wakati wa mahojiano na vyombo vya habari nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya wabunge kuitaka serikali itoe tamko kutokana vitendo ya utekaji na kuchukuliwa watu kuendelea kujitokeza nchini.
“Tayari wizara yangu inashughulikia suala hilo la kutekwa msanii Roma Mkatoliki na kuchunguza ili kuona ni nani anahusika katika utekaji huo, kwani anaweza kuwa asiwe askari na mtu mwingine akatumia mavazi ya askari kufanya utekaji huo,’.
Mwigulu amesema kama serikali kupitia wizara yake inatakiwa kufanya mambo kwa uhakika pamoja na kuchunguza ndipo itoe taarifa kuhusu jambo lolote.
Waziri huyo amesema kuwa tayari wizara yake imechukua hatua za kuchunguza jambo hilo la msaniii Roma ambaye aliyetekwa na wanzake wakiwa katika studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.