Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kuwa Serikali haihusiki na mkataba wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoingia na Benki ya CRDB kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali, utaratibu wa tiketi hizo ulipoanza TFF iliingia mkataba na CRDB lakini baada ya huduma hiyo kuingia dosari, Serikali iliingilia kati na kutaka huduma isimame mpaka changamoto zilizojitokeza zitakapotatuliwa.

Waziri Nape alikutana na waandishi wa habari jana kwenye Uwanja wa Taifa kikao kilichokuwa maalumu kwa ajili ya kuwaelekeza matumizi ya mfumo huo utakaoanza kutumika rasmi Oktoba Mosi.

Waziri Nape amesema serikali haiusiki kwa kuwa wakati TFF inaingia mkataba na benki hiyo walikuwa hawafahamu hivyo anawaacha wamalizane wenyewe.

Nape amesema kukamilika kwa mashine hizo za elektroniki, serikali haikutumia gharama zake isipokuwa zilitakiwa kuwepo tangu kwenye ujenzi wa uwanja huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *