Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, leo ameweka jiwe la msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.

Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.

Amesema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

Amewapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.

Amesisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.

Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *