Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amezindua kiwanda cha kutengeneza viungo mbali mbali vya chakula wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kiwanda hiko kinachoitwa Vegata Podravka Ltd kimetengenezwa na kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 mpaka kukamilika kwake.
Waziri Mwijage ameishukuru kampuni hiyo kwa kutengeneza kiwanda hicho na kuwataka wawekezaji kujitokeza kutengeneza viwanda vingi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano kuhusu viwanda.
Uzinduzi huo pia umeudhuriwa na mbunge wa Bagamoyo, Shukuru Kawambwa ambapo mbunge huyo ameshukuru kujengwa kwa kiwanda hiko kutokana na kukuza sekta ya viwanda nchini.
Kiwanda hiko kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 200 kwa wakazi wa Bagamoyo zikiwemo kazi za kusambaa bidhaa za kiwanda hiko.