Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuanzia sasa mtu yoyote mwenye majeraha atapata matibabu hospitali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi (PF3) kama ilivyozoeleka hapo awali.

Mwigulu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook kwa kusema utaratibu huo unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili kubaini ukweli wa jeraha la muhusika.

Kupitia akaunti yake ya Facebaook Mwigulu ameandika “Tumeamua majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3”.

Pia ameongeza kwa kuandika “Hatua za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalengea kuokoa maisha yao kwanza, utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika”.

Waziri Mwigulu ameamua kueleza jambo hilo baada ya Jeshi la Polisi kutupiwa lawama nyingi kutoka kwa wananchi kuhusu PF3.

Lawapa hizo zimetolewa na watu ambao wamepatwa na matatizo na kushindwa kupewa huduma hospitali kwa haraka mpaka wapitie kituo cha Polisi kupatiwa cheti cha PF3 ili aende kupata huduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *