Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema hajasitisha mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki nchini bali ametoa angalizo kwa waandaaji wa mashindano hayo kuwa na uhakika wa kuyaendesha mashindano hayo.

Mwakyembe amesema hayo jana kwenye ziara yake mjini Mtwara baada ya taarifa kuenea kuwa amefuta mashindano hayo.

Mwakyembe yuko mkoani Mtwara katika ziara ya kuzungumza na watendaji walio chini ya wizara yake na kuzungukia viwanja vya michezo.

Amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la uendelezaji, hivyo ametoa agizo kwa Baraza la Sanaa (Basata) kwamba mtu yeyote akija na shindano au wazo la tuzo watamruhusu pale tu atakapotoa msingi wa mwendelezo na siyo kwa kuwa amepata mfadhili wa muda.

Pia Mwakyembe amesema amekuwa akifuatwa na warembo kadhaa ofisini kwake wakilalamikia kutopewa zawadi zao mara baada ya mashindano ya Miss Tanzania kumalizika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *