Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe amepata msiba wa kufiwa na mke wake Bi Lina George Mwakyembe usiku wa kuamkia tarehe 15 Julai, 2017.

Bi. Linah alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Agha Khan alipokuwa akipatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta.

Shughuli za msiba huo zinafanyika nyumbani kwa waziri Mwakyembe, Kunduchi Beach karibu na chuo cha mafunzo ya kijeshi jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *