Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amefukuza kazi Naibu wake, Damian Green baada ya kugundulika alidanganya kuhusu kwa video za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya bungeni
Uchunguzi kwenye ofisi ya baraza la mawaziri ulisema alitoa taarifa ambazo sio sahihi na za kupotosha akikataa kuwa alijua kuhusu kugundulika kwa video hizo kwenye uvamizi wa polisi kwenye ofisi za bunge mwaka 2008.
Green alilazimishwa kujiuzulu baada ya washauri kwenye masuala ya mawaziri kusema alivunja maadili ya uwaziri.
Green alikuwa mshirika mkubwa wa waziri mkuu, na kuondoka kwake kutakuwa ni pigo kubwa kipindi hiki ambacho Uingereza inapitia kwenye majadiliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya.