Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania iko tayari kujifunza kutoka kwa nchi nyingine ambazo ni wanachama wa Mpango wa Kujitathmni Kiutawala Bora barani Afrika (APRM) ili iweze kuboresha hatua ilizofikia kwenye mpango huo.

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo wakati akichangia mada katika Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Mpango wa Kujitathmni Kiutawala Bora barani Afrika (APRM Forum) uliofanyika kwenye hoteli ya InterContinental jijini Nairobi nchini Kenya.

Waziri mkuu amesema kwamba Tanzania imeshaanza kutekeleza mpango kazi wa Kitaifa ambao umejikita kutatua changamoto katika sekta za maji, elimu, kilimo, nishati na miundombinu kama zilivyoainishwa kwenye kikao cha APRM.

Tanzania ilifanyiwa tathmini yake Januari, 2013 kwenye kikao cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Viongozi: Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano nchini Kenya.
Viongozi: Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano nchini Kenya.

Kwa upande mwingine Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati akifungua kikao hiko amesema kwamba viongozi wa Afrika hawana budi kukubaliana na kuungana kutafuta suluhisho katika ushindani wa kibiashara.

Pia amesema nchi wanachama wa mpango huo hawana budi kujenga umoja kama njia ya muafaka ya kufikia makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *