Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hali ya chakula nchini kwa sasa hairidhishi.
Majaliwa ametoa kauli hiyo jana wakati akihitimisha shughuli za mkutano wa saba wa Bunge la 11 mjini Dodoma.
Akizungumzia hali ya chakula nchini, Waziri Mkuu amesema bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula.
Majaliwa amesema hata hivyo, kuna maeneo yaliyopata mvua nyingi na chakula cha kutosha.
Waziri Mkuu amesema kwa baadhi ya maeneo mazao ya chakula na hasa mahindi yameanza kushuka bei katika masoko.
Amesema licha ya upungufu wa chakula katika nchi zinazoizunguka Tanzania, Serikali imepiga marufuku usafirishaji wa mahindi nje ya nchi bila kibali.