Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali na kuacha kufanya mambo yasiyokuwa na tija katika uchumi na maisha ya kila siku.

Majaliwa ameyasema hayo mjini Dodoma katika uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gauge kutokea Morogoro mpaka Makotopora, ambapo Waziri Majaliwa aliwasihi Watanzania kuwa watulivu kusubiri utekelezaji.

Amesema kuwa “Nawasihi Watanzania wote kuwa watulivu kusubiri utekelezaji lakini kushiriki kikamilifu katika kujenga ujenzi wa miundombinu hii ili tuweze kupata manufaa”.

Ameendelea kusema “Nataka niwasihi Watanzania nikianza na hii reli yetu, reli hii ni fursa kwetu sote tunaopitiwa na reli hii kutoka Dar, Mwanza, Kigoma kupitia hapa Dodoma”.

Pia amesema kuwa “Ndugu Watanzania nataka niendelee kuwasihi tuachane na mambo ambayo hayana tija kwa uchumi wetu na kwenye maisha yetu ya kila siku tuendelee kuhamasishana kuunga mkono shughuli za maendeleo kila mmoja ajitoe kuunga mkono jitihada za serikali.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *