Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka vijana kuchangamkia fursa kwa kuandaa mitaji ya kuwa na gereji za kuchomelea vyuma.

Majaliwa amesema hayo mkoani Lindi ambapo ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa humo.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi katika vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho, alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na ku,uagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-Mibure.”

Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa k, saluni na viwanda vidogo vya usindikaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *