Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa amesema kuwa Serikali itapambana na janga la madawa ya kulevya kwa dhati bila kumuonea mtu yoyote na kuzingatia misingi, sheria na haki.

Kauli hiyo ameitoa jana Bungeni wakati akitoa hoja ya kuhairisha mkutano wa sita bunge la 11 mkoani Dodoma.

Waziri mkuu amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale warioathiri ambao ni wauzaji na wasambazaji wa dawa hizo hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa takwimu za jumla zinaonesha kuwa watanzania waliokamatwa ni 515 na wamefungwa katika magereza ya nchi mbali mbali kutokana na makosa hayo ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Pia Waziri mkuu amezitaja nchi ambazo watanzania wamefungwa kutokana na biashara hiyo ni China ambapo wapo watanzania 200, Brazil wamefungwa 12, Iran wapo 63, Ethiopia wapo saba na Afrika Kusini wapo watanzania 296.

Waziri mkuu ameunga harakati za kupambana na madawa ya kuelvya zilizoanzishwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kuwataja wahusika wa biashara hiyo hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *