Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua mkutano wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili ya Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,Waziri Majaliwa amewapongeza wakuu hao ambapo amewataka kuhakikisha wanaongeza juhudi na maarifa katika mashirika yao ili kusonga mbele.
Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu hao kuongeza ubunifu zaidi ili kuongeza maarifa katika mashirika yao hii ni pamoja na kujiendesha kwa faida ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kujiendesha.
Majaliwa amelipongeza Shirika la Nyumba NHC ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa likiendeshwa kwa hasara, hata hivyo baada ya kuongeza ubunifu na kuingia kijana mzawa, wameweza kupiga hatua na sasa wamekuwa wa mfano wa kuigwa.
Majaliwa amesema mpaka sasa Serikali imeweza kuwa na Mashirika ya umma 264 ambapo kati ya Mashirika hayo, Mashirika 65 ni Mashirika ya Kibiashara, Mashirika 187 ni mashirika ya huduma wakati mashirika 12 ni udhibiti.