Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameongoza mazishi ya mama yake mdogo rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Bi Nuru Kikwete jana.
Viongozi wengine wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Waziri mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na waziri wa mambo ya nje wa zamani, Benard Membe.
Mazishi hayo yamefanyika Bagamoyo mjini mkoani Pwani nyumbani kwa marehem mida ya saa saba mchana.
Bi Nuru Kikwete ni mke wa pili wa baba mzazi wa Kikwete alifariki siku ya jumanne katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabo.