Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Wakati wa kukabidhi pikipiki hizo Waziri mkuu amewataka waendesha madereva wa pikipiki hizo wahakikishe wana leseni na bima.

Waziri Majaliwa amekabidhi pikipiki hizo jana baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *