Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amezitaka idara zote zilizo chini ya wizara yake kutumia fedha za ndani katika miradi yake ili kujenga misingi ya kujitegemea na kutokufikiria mikopo.

Prof. Mabarawa ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati wa utiaji saini wa ununuzi wa mradi na ufungaji wa rada nne za kiraia ambao unatekelezwa kwa fedha za serikali.

Amesema kuwa “Natoa wito kwa taasisi zote ambazo zina fanya miradi hasa kwenye wizara yetu tusifikirie kwanza mkopo tuangalie jinsi gani tunaweza kujipanga ndani kuweza kukusanya mapato mazuri ili tuhakikishe pesa hiyo tunaitumia kufanya mradi husika,”.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Sekta ya utalii sasa kwasababu mashirika mengi hata nje yatajua anga zetu zipo salama kwa vile ndege nyingi sana zitaleta utalii nchini na utalii utakuwa sana.

Pia amesema kuwa utalii ukikuwa maana yake nini uchumi wetu unaongezeka pesa za nje zinaongezeka na ajira zinaongezeka,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *