Waziri wa mambo ya Nje ,Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda Dkt. Augustine Mahiga ameagiza watendaji wa wizara hiyo kuacha kuandika vitu kwa makisio hali inayofanya utekelezaji wake kuwa mgumu hali inayopelekea watu kukosa imani na serikali.
Ameyasema hayo jana kwenye kikao cha pamoja na maafisa mbalimbali wa wizara hiyo ambapo amesema agizo hilo litekelezwe kanzia mwaka huu wa fedha 2018/2019 ili kujipima utekelezaji wa kazi zao unakwendaje nakufanyia kazi maeneo ambayo hayajafikiwa.
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara hiyo Dkt.Adolf Nkenda amesema wamefanya mabadiliko makubwa katika idara mbalimbali ili kubaini mapungufu yalipo ikiwa ni pamoja na utoaji haki kwa wafanyakazi kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya upendeleo na matabaka wizarani hapo.
Katika tukio lingine Dkt.Mahiga alimuongoza waziri wa mambo ya nje ya shirikisho la Ujerumani Mh. Heiko Maas kuweka shada la maua kwenye sanamu ya askari eneo la Posta ikiwa ni ishara ya kumbukumbu kwa Ujerumani na Tanzania na baadae kufanya kikao cha ndani na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.