Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameahidi kusimamia uimarishwaji wa uhusiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Korea Kusini ili wananchi wa pande zote mbili wapate manufaa.

Waziri Mahiga ameyasema hayo alipokuwa anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ambapo siku ya mwisho aliitumia kikamilifu kukutana na taasisi za umma za biashara na viwanda, Benki ya Exim ya Korea pamoja na makampuni binafsi yanayojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.

Amesema kuwa miaka 25 ya kwanza ya uhusiano wetu na Jamhuri ya Korea ilijikita kwenye kuweka misingi imara ya uhusiano wa kidiplomasia ambapo nchi zetu zilikuwa zinajiimarisha kama mataifa huru.

Bw. Chang Yaong Hun, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim ya Korea, Mheshimiwa Mahiga mbali na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa mikopo na misaada nchini Tanzania, Waziri Mahiga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli sasa imejikita kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ujenzi wa viwanda ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu. Kwasasa Benki hiyo inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na maji mikoa mbalimbali ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *