Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la  Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.

Waziri huyo pia  amewataka  watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa.

Amesema  hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi  kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe.

Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai  Januari mosi ataenda  tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *