Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.
Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo yote yote Nchini.
Niwapongeze baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.
Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya kuheshimu mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini, kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Awali akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa mafunzo haya yanakamilisha mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia Viongozi 324.
Prof.Semboja aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade ya Jamii Tunayoihudumia.