Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali ya nchi yake.
Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege.
Waziri huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un.
Mapema mwezi huu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Korea Kusini.