Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekagua miundombinu mkoani Dodoma kwa ajili ya sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baada ya ukaguzi huo Waziri mkuu amesema kuwa miundombinu imekamilika na maandalizi ya sherehe hizo yako pazuri.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumatatu mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi na kukagua Uwanja wa Jamhuri ambapo sherehe hizo zitafanyika na uwanja wa Nyerere Square.

Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi kutoka wilaya zote za mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani wafike kwenye maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania yanafanyika mkoani humo.

Sherehe hizo zitahudhuriwa na wageni mbali mbali ndani na nje ya nchi pamoja na wake wa viongozi wasisi wa Taifa hili, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *