Wakala wa Wayne Rooney, Paul Stretford yupo nchini China kufanya mazungumzo ili mchezaji huyo kuhamia klabu ya Ligi Kuu ya China.

Bado hakuna mafanikio na duru zinasema huenda ikawa vigumu kwake kufanikiwa kuhamia huko kabla ya muda wa wachezaji kuhama China kumalizika tarehe 28 Februari.

Stretford amesafiri China ni ishara wazi kwamba meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anaweza kumwacha Rooney mwenye umri wa miaka 31 ahame.

Rooney ameshuka hadhi United chini ya Mourinho na amekuwa hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi.

Nahodha huyo wa England alifahamishwa mapema kwamba anatafutwa na klabu za China, ingawa haijabainika ni klabu gani zinamtaka.

Kutokana na masharti yaliyowekewa klabu za China kuhusu wachezaji wa kutoka nje, klabu za Jiangsu Suning na Tianjin Quanjian ndizo pekee zinazoonekana kuwa na nafasi ya kutaka kumnunua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *