Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma amesema wamekabidhi jumla ya Sh milioni 30 ikiwa ni sehemu ya fedha za mchango wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi zilizokusanywa kwa ajili ya watu wali Mgeni Hassan Jumaiopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Mgeni amesema fedha hizo zinatokana na michango ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao walijitolea kukatwa posho ya siku moja ya kikao cha Baraza kwa ajili ya kuchangia watu walioathirika na tetemeko la ardhi Kagera.

Amesema msiba uliowapata wananchi wa Kagera ni janga la kitaifa ambalo linaweza kuwaathiri pia wananchi wa Zanzibar ambao ni ndugu wakitoka katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Mgeni alitumia nafasi hiyo kutoa rambirambi kwa wananchi wa Kagera na kuwataka kuwa na moyo wa subira na ustahamilivu huku wakijua kwamba maafa hayo ni ya watu wote.

Amesema majanga ya kimaumbile kwa kawaida hayatabiriki kwa sababu ni ajali ambayo hupangwa na Mwenyezi Mungu kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuwa na subira ya hali ya juu.

Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ukiongozwa na Naibu Spika ulipata fursa pia ya kuwatembelea watu waliopata maafa hayo ambapo wengi nyumba zao na makazi ya kawaida yameathirika vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *