Watu wawili wamefariki wakati wakibatizwa siku ya Jumapili, kwenye mto ulio eneo la Rombo mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa naibu kamanda wa polisi Hamisi Selemani Issa, watu hao walikuwa wakibatizwa kwa kuzamishwa ndani ya maji, katika zoezi lililokuwa likiendeshwa na mhubiri wa Kanisa la Shalom huko Rombo.

Walizama maji katika mto Ungwasi wakati walikuwa wakizamishwa baada ya kile kinachotajwa kwa kulemewa na mawimbi makali ya mto huo.

Haijulikani ni kwa njia gani mhubiri na waumini wengine waliokuwa wakiendesha zoezi hilo walinusurika.

Naibu kamanda wa polisi amesema kuwa waumini wa kanisa akiwemo pia mhubiri wamezuiliwa ili kuhojiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *