Watu watatu wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali ya basi la kampuni ya Mohemed Trans lililogonga lori na kupoteza mwelekeo katika mji wa Manyoni mkoani Singida.
Basi hilo lilikuwa limekodiwa na walimu ambao walikuwa wakisafiri kutoka jijini Tanga.
Chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo lililokuwa limeegeshwa barabarani bila tahadhari yoyote, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari limepaki na yeye akatanua kwa haraka.
Wakati huohuo, basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendokasi hivyo kuligonga lori la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichosababisha kumwagika mafuta barabarani licha ya kwamba hayakushika moto.