Watu sita wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia mtaa mmoja mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Gavana wa jimbo la Mandera Ali Roba ameandika kwenye Twitter kwamba watu 6 wameuawa na mmoja kujeruhiwa.

Eneo la Mandera limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wa al-Shabaab kutoka Somalia.

Kenya ilipeleka vikosi vyake vya jeshi nchini Somalia mwaka wa 2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara na kuisaidia serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kundi la al-Shabab mara kwa mara hutekeleza mashambulio nchini Kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka wa 2013.

Mwezi Juni mwaka huu, wanamgambo wa kundi hilo walishambulia gari ya polisi aina ya Land Cruiser kilomita chache kutoka mji wa Mandera.

Mwaka uliopita al-Shabab walitekeleza mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *