Watu saba wamekamatwa katika uvamizi mjini London na Birmingham kufuatia shambulio la la kigaidi Westminster lililowauwa watu watano.
Mamia ya polisi wa upelelelezi wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha wakifanya uchunguzi dhidi ya makazi sita, amesema kaimu naibu wa kamishna wa polisi Mark Rowley.
Wale waliokufa walikuwa ni mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40, mwanamume mwenye miaka 50 Polisi Keith Palmer pamoja na mshambuliaji, aliongeza.
Saba miongoni mwa majeruhi bado wako hospitalini katika hali mahututi.
Wengine 29 zaidi wamekuwa wakipata matibabu hospitalini, ameongeza Rowley.
Katika shambulio la Jumatano, mwanamume mmoja aliendesha gari kwenye njia ndogo karibu na Westminster na kuwagonga wapitanjia, huku akiwaacha kadhaa na majeruhi.
Kisha alimpiga kisu kisu polisi na akapigwa risasi na polisi kwenye eneo la bunge nchini humo.