Watu 64 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi.
Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41 kutokana na ajali hiyo ya moto katika jingo hilo.
Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka.
Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka nje kupitia madirisha kujaribu kujinusuru kutoka kwa moto huo uliozuka Jumapili.
Wazima moto zaidi ya 660 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji ambapo chanzo cha moto huo hakijabainika lakini maafisa wameanzisha uchunguzi.
Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametuma salamu zake za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathiriwa, sawa na Waziri wa mambo ya nje wa Latvia Edgars Rinkēvičs.
Kando na kumbi nyingi za sinema, jumba hilo, ambalo lilifunguliwa mwaka 2013, lina migahawa kadha, na vituo kadha vya bafu za maji ya mvuko, kito cha mchezo wa bowl na kituo cha kujumuika na wanyama.