Mvua kubwa iliyonyesha maeneo hayo imesababisha kufurika kwa mto Kalamu, ambao ulimwaga maji katika mji wa Boma, ulipo pasuka kingo zake Jumanne.
Miili ya waliokufa ilisombwa kwa maji hadi nchi jirani ya Angola, amesema gavana wa eneo hilo.
Gavana wa jimbo la Congo ya kati amesema kuwa mara ya mwisho yalitokea mwezi Januari 2015, lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yametokea sasa mwezi Disemba 2016.
Maji ya mto Kalamu yalijaa kimo cha mita mbili (futi sita) juu ya kimo chake cha kawaida , aliongeza.
Mafuriko makubwa, ukame na gharika vinatarajiwa kuongezeaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi baran Afrika.