Watu 340 wamefariki dunia nchini Iran na Iraq kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 katika nchi hizo.

Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka manyumbani mwao kwenda barabarani.

Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.

Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi la lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.

Uharibifu umeripotiwa kuetka katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.

Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa

Tetemo hilo lilitokea kilimita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *