Mlipuko umetokea jijini New York, katika eneo la Chelsea, Wilaya ya Manhatan ambapo watu 29 wamejeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.

Polisi wanashuku huenda mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi na wanaendelea na uchunguzi kubaini ukweli wa mambo.

Meya wa New York, Bill de Blasio amesema mlipuko huo ulisababishwa kwa makusudi lakini akasisitiza kuwa hadi sasa haujahusishwa na kundi lolote la kigaidi.

Amesema pia kuwa hakuna ushahidi kuwa mlipuko huo una uhusiano wowote na bomu la mfereji lililolipuka katika jimbo jirani la New Jersy saa chache zilizopika.

New York: Eneo la lilipotokea tukio la mlipuko wa bomu na kusababisha majeruhi 29.
New York: Eneo la lilipotokea tukio la mlipuko wa bomu na kusababisha majeruhi 29.

Bomu hilo lililipuka karibu na mahali ambapo mbio za kukusanya pesa za kuwasaidia wanajeshi wa zamani zilikuwa zikiendeshwa.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanahisi kwamba uhenda likawa shambulio la kigaidi lakini bado alijathibitishwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *