Makundi ya uokoaji yamefika katika eneo la tukio kutoa msaada na watu wametahadhalishwa kutosogea katika eneo hilo na barabara kuachwa wazi.
Gavana wa eneo hilo Eruviel Avila amesema kuwa kwa sasa nguvu kubwa imeelekezwa kusaiia majeruhi na watoa huduma wa serikali wamepelekwa katika eneo hilo
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa idadi ya milipuko iliendelea ada ya mlipuko wa kwanza na hatimaye oshi mkubwa na moto ukafunika anga.
Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto kupitia ukurasa wake wa Tweeter ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mlipuko huo na majeruhi
Soko hilo la fataki la San Pablito mwaka 2005 lilikumbwa na mkasa kama huo baada ya mfulilizo wa milipuko na moto mkubwa ulipozuka wakati taifa ilo liijiandaa kwa sherehe za uhuru.