Watu 17 wamefariki Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Visa 21 vya homa na kutokwa na damu, pamoja na vifo 17 vimeripotiwa katika jimbo la Equateur.

Hii ni mara ya tisa kwa maradhi hayo kutokea nchini Congo tangu mwaka wa 1976, wakati kulipogundulika kwa mara ya kwanza virusi vya ugonjwa huo.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limesema mjini Geneva kwamba, vipimo vya maabara vimethibitisha uwepo wa virusi vya Ebola katika sampuli mbili kati ya tano za wagonjwa.

WHO wamesema kuwa tayari wamepeleka kiasi cha dola Milioni 1, kutoka mfuko wa dharura na wataalamu zaidi ya 50 watakaoshirikiana na serikali na taasisi za afya, kukabiliana na ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *