Watu 15 wameuawa nje ya kambi ya jeshi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya bomu kutegeshwa kwenye gari.

Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab limekiri kufanya shambulio hilo siku ya Jumapili asubuhi, huku wakimlenga kiongozi wa jeshi la Somalia.

Hili ni tukio la hivi karibuni katika kampeni za wapiganaji hao ambalo inaendelea kuhatarisha usalama wa nchi.

Shambulio hilo limeharibu magari na kujeruhi watu karibu na wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.

Mlipuko huo ingawa ulilenga msafara wa maafisa wa ngazi za juu wa jeshi, lakini idadi kubwa ya waliojeruhiwa ni wananchi wa kawaida waliokuwa karibu kwenye gari.

Shambulio hilo linatokea wiki moja tu baada ya Rais wa Somalia Mohamed Farmajo kutangaza vita dhidi ya Al Shabaab lakini pia kutoa siku 60 kwa wapiganaji watakaotubu.

Kundi hilo limesema kauli hiyo ya Rais ilikuwa na lengo la kuridhisha nchi za magharibi.

Vitisho vya Al Shabaab vimeendelea kwa mwezi wa pili tangu Rais Farmajo kuingia madarakani, huku wapiganaji hao wakilengo maafisa wa serikali na vikosi vya Umoja wa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *