Zaidi ya watu 100,000 wamekumbwa na njaa huku wengine zaidi ya milioni moja wakiwa kwenye hataia ya kukumbwa na njaa nchini Sudan Kusini.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuporomoka kwa uchumi vyote vimechangia kuwepo hali hiyo.
Kumetolewa onyo la kutokea njaa nchini Yemen, Somalia na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria lakini Sudan kusini ndio ya kwanza kutangaza njaa.
Ukosefu wa chakula kwa sasa unakumba maeneo ya jimbo la Unity nchini Sudan Kusini lakini makundi ya kutoa huduma za kibinadamu yameonya kuwa hali hiyo itasanbaa kiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.
Mashirika ya kutoa misaada yakiwemo ya WFP na Unicef yamesema kuwa watu milioni 4.9 ambao ni zaidi ya asimia 40 ya watu wa Sudan Kusini wanahitaji chakula kwa dharura.