Watu tisa wameuawa mjini Toronto, nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea katika mtaa wenye watu wengi.
Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi.
Diego de Matos yeye alikuwa akiendesha gari lake karibu na eneo hilo,ameiambia BBC kuwa aliona watu wawili wakigongwa na gari hilo la mizigo.
Waziri wa usalama wa Canada Ralph Goodale amewaambia waandishi wa habari kwamba ni mapema kusema tukio hilo ni la kigaidi.
Kumekuwa na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi kusababisha vifo katika maeneo yenye mikusanyiko,baada ya mamlaka za usalama kudhibiti njia za magaidi hao zilizooeleka.
Matumizi ya magari makubwa ya mizigo,ni mfumo mpya ambao umekuwa ukitumiwa na magaidi kutekeleza azma yao kufuatia kubainika kwa njia zao zilizo mara zote.