Watanzania wanane waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ujasusi nchini Malawi wameachiwa huru.

Watanzania hao, waliachiwa baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikiwakabili, iliyotolewa hukumu juzi jioni na kuonekana hawana hatia.

Walikuwa wanashikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani uliopo eneo la Kayerekera.

Serikali ya Tanzania ilikataa kwamba Watanzania hao walitumwa ili kufanya shughuli za kijasusi katika mgodi huo.

Ilisema kuwa walikuwa wafanyakazi wa Taasisi ya Misaada ya Caritas iliyo chini ya Kanisa Katoliki, Jimbo la Songea mkoani Ruvuma.

Wakili aliyekuwa anawatetea katika kesi hiyo, Flaviana Charles, alisema wateja wake wameachwa huru ingawa wamepitia wakati mgumu.

Amesema wakati wanawakamata walikuwa hawajafika mgodini, kwa sababu walikuwa hotelini walikokuwa wamefikia.

Wakili Flaviana, alisema kuna ujanja ambao mahakama iliutumia ili kukwepa fidia kwa kudai tayari wametumikia kifungo kipindi hicho chote walichokuwa wameshikiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *